HONGERA SANA KAKA VICTOR J. MSHANA
Iliwashangaza wengi pale kaka yetu
Victor Mshana alipotangaza kuwa amepata mchumba. Wengi walifurahia sana. Lakini
iliwashangaza wengi wengi pale alopseama anataka kuoa rasmi.
Basi, maamuzi aliyoyachiukua Victor
yalipongezwa sana hasa marafiki zake na familia kwa ujumla pale Victor
aliptamka rasmi kwa baba yake mzee Msahana…..’’Baba, nimepata mchumba, na kwa
umri huu nataka niachanae na ukapera na niwe na familia yangu niishi kama mme
na mke….’’
Baba akakubali maana imeandikwa …Mtoto
atamwacha baba na mama yake, na ataambatana na mkewe na kuishi kama mke na mme.
Ndipo tarehe 20.02.2016 ilikuwa siku ya kipekee kwa kaka yangu Victor Mshana alipoudhihilishia ulimwengu kuwa yeye na ukapera BYE! BYE!
Ni siku hiyo Victor bila kupepesa macho wala kuogopa
aliyatamuka maneno haya mbele ya waumini na mbele ya mchungaji….’Mimi Victor
Mshana, nakubali kumuoa …………..ili awe
mke wangu wa ndoa, nitaishi nae katika shida na raha, ugonjwa na afya, utajili
na umasikini….. hadi kifo kitutenganishe.
Uriiiiiiiiii, Uriiiiiiii, Uriiiiiiii……. Ni sauti za
vigeregere zilizosikika kutoka kwa waumini pale Victor alipoitumbukiza pete
kwenye kidole cha bi harusi na bi harusi naye akaitumbiukiza pete kwenye kidole
cha Bwana harusi ambae ni Victor
Baada ya ndoa kanisani, tukio lilifouta nyuma lilikuwa la
kipekee, vijana wakajimwaga kuchukua picha za matukio.
Ni katika sanamu ya mnyama aina ya Faru, kama sehemu ya wanyama waa kitalii nchini Tanzania, basi bwana na bibi wakasema tukachuke picha hapa kwenye sanamu ya mnyama huyu
Ni katika jengo la ghorofa ya 16 jengo lefu sana, basi bwana na bibi wakasema kwanza tupande huko juu ili tuone chini panaonekaje. Chini wakaona uwanda mzuri wa Tanzania mjini Arusha, ukingaa nao wakafurahia upepo mzuri na mwanana
Ni katika uso wenye furaha katika bustani iliyoandaliwa mahususi kwa hawa wawili, yaani Mr and Mrs
Mrs akaamua kumbeba mgongoni Mr. Mbereko ndiyo ilikosekana, lakni Mr alibebwa kama ujuavyo......
...Nyanyuka mama, wewe ndo kila kitu, nimekusotea mda mrefu (Mr akimwambia Mrs)
Maakuli hayo nyuma ya bwana na bibi harusi. Ndafu ilikuwepo, pilau, wali mweupe, kachumbali. Watu walikula haoo, wakanywa, wakacheza, sema ni wewe tu uliyekosa, lakini tukio lilifana kweli
Vijana wenzake bwana harusi wakimjoki kwa nyuma, wakimkumbusha ya nyuma hadi bwana na bi harusi wakashtukia washaangua kicheko. Mambo ya vijana hayo.
Ilikuwa ni siku ya
kipekee kwa kaka Victor Mshana. Kwa niaba nzima ya vijana wenzako,
tukutakie maisha yenye baraka na amani. kwa zawadi ya kipekee,
tunakuzawadia biblia ewe Bwana harusi, soma sana biblia, umo ndo kuna
maarifa ya jinsi ya kumtunza mkeo na kuitunza famila. N a kwako Bi
harusi, tunakuzawadia kitabu cha Tumwabudu Mungu Wetu, imba sana, mmeo
hata akiwa mkorofi kiasi gani, wewe imba tu.













0 comments:
Post a Comment