
HUKUMU IMETOLEWA. JE, TUNAJIFUNZA
NINI KUTOKANA NA MSICHANA WA KAZI (MIAKA 22) KUMTESA MTOTO WA MIEZI 18?
Katika
mwezi wa 11 mwaka huu wa 2014, mitandao yote ya kijamii na vyombo vyote vya
habari viliandika juu ya binti wa kazi huko nchini Uganda kumtesa mtoto
mchanaga wa miezi 18. Wengi walilaani kitendo cha huyu binti alichokifanya kwa mtoto
mchanga. Na zaidi wengi walisema ahukumiwe kifungo cha maisha jera au auawe kwa
unyama alioufanya.
Ilikuja
kugundulika baada ya mwenye nyumba(baba wa mtoto) kuona kwenye kamera ya ulinzi
iliyofungwa kwenye nyumba yake, ndipo akampa kichapo binti wa kazi na binti
akaamua kukimbilia polisi, baba mwenye nyumba alipokamatwa akaelezea kisa cha
kumpga binti huyo na video akaitoa kama ushahidi. Ndipo kibao kikamgeukia binti
wa kazi na kuwekwa rumande akisubilia hukumu ya kutaka kuua kwa kukusudia.
Wiki
moja baadae nilishangaa kukuta katika chombo kimoja cha kimataifa kimeandika
kuwa Saudi Arabia imekataza raia wake kuajili Mayaya(wasichana wa kazi toka
Uganda) kulingana na kitendo cha binti wa kazi wa Kiganda alichomfanyia mtoto
mchanga. Mara hii jamani? Kosa amefanya mtu mmoja lakini jamii nzima ya Uganda
imehukumiwa (Do not generalize)
Ni
sawa binti wa kazi alikuwa na kesi ya kujibu ambayo iko wazi kwa kila mtu na
ushahidi ukiwa unajionesha waziwazi bila chenga. Na wengi wao walitoa hukumu
zao, wengine wakisema afungwe maisha jera, wengine wakitaka auawe. Ilimradi
kila mwenye mdomo alisema kilicho chake na weye uwezo wa kuandika waliandika
kama walivyoona.
Ni
ukweli usiopingika kuwa binti alifanya kosa, na kosa kubwa, na Madakitari
walimpima na kukuta ana akili timamu lakini kuna binadamu yeyote ambaye
amejiuliza walau maswali mawili juu ya huyo binti?
Tunaposoma
biblia tunaona Mwenyezi Mungu alituumba wanadamu wote tukiwa wakamilifu, na
tukirudi kwa upande mwingine(Sociological Analysis) tunaona kuwa baada ya
kufika duniani, mwandadamu anakutana na mazingira mapya, watu wapya na mengine
mengine ambayo yanamzunguka na kufanya ukamilifu wake upotee na kuwa mpya
katika mazingira yanayomzunguka (socialization)
Nikirudi
pale pale kwa binti wa kazi na kitendo chake alichokifanya, ni kweli ni kosa
kubwa na nazidi kusema ni kosa kubwa sana, lakini hatukupaswa kumhukumu haraka
sana kwa kitendo chake alichokifanya na uthibitisho wa madakitari kuwa ni mzima
wa akili. Tunapaswa kuangalia historia ya binti huyu, na familia anayotoka.
Kiubinadamu,huenda kuna jambo lilimuumiza huko nyuma, nayeye bila kujua hasira
akazimalizaia kwa mtoto mchanga(tena bila kujua kuwa anafanya makosa). Ni wengi
sana tumeshuhudia wapenzi wakisalitiana na wengine wanachukua maamuzi ya gafla
mfano kupasua kitu, kuchana nguo au hata kujiua. Haya yote ni historia ya kitu fulani
na mwishowe wengine hujutia. Ndivyo ilivyo kwa huyu dada wa kazi.
Mimi
nadhani pamoja na hukumu yake ya kutaka kuua kwa kukusudia, pia ningependa
wanasociologia na wanasaikolojia wangeongea na huyu binti ili kujua behind the
incidence kuna nini. Najua kuna kitu nyuma ya pazia kimejificha.
Yametokea
hayo na tunamshukuru Mungu mtoto mwenyewe hajafa, amepona majeraha na ni mzima
wa afya. Je, wazazi tunajifunza nini kutokana na hili lililotokea? Waswahili
wanasema leo kwangu, kesho kwako. Kama huyu mtoto amejeruhiwa vibaya, jua wa
kwako ndo utamkuta kabanikwa kwenye moto.
Ni
vizuri wazazi kama munataka kuleta wasaidizi wa kazi kuweni makini nao, walau
kwa kujua historia ya maisha yao, na familia wanakotoka. Pia wazazi ishi na
wadada wa kazi vizuri kwani wengi wao wanateswa na waajili wao hivyo wanaamua
kulipiza kisasi kwa hayo wanayotendewa.
Pamoja
na hiyo, kama mna mtoto mchanga na nyie wazazi nyote ni waajiliwa ni vizuri
mkawa na utaratibu mzuri wa kulea mtoto wenu kama kuomba ruhusa ya kufanya kazi
za ofisi ukiwa nyumbani kwako huku ukilea mtoto wako, au kumpeleka mtoto kwenye
vituo vinanyoaminika vya kulea watoto wadogo(day care centre), au kuajili bibi
wa mtoto kulea mjuu wake.
Asanteni sana na siku njema.





0 comments:
Post a Comment