Ndege ya kwanza ya ATCL yatua nchini
Ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa ajili ya kutumiwa na shirika la ndege la TANZANIA (ATCL), imetua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl JK ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa
Ndege hiyo aina ya Bombadier Q 4000 NextGen imetua majira ya saa 6:15 mchana na kisha kupatiwa heshima maalumu ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya inapotua katika nchi yake (Water Salute)
Baada ya kupokea heshima hiyo, ndege hiyo imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing Ukonga)
Ndege ya pili itatua nchini baada ya wiki moja, na baada ya ndege hiyo ya pili kuwasili, yatafanyika mapokezi rasmi yatakayoongozwa na Mh Rais.
Shime kwa watanzania, tuwe tayari kwa usafiri wa anga tena wa uhakika kwa kutumia ndege zetu wenyewe aina ya Bombadier Q4000.
0 comments:
Post a Comment