LIFAHAMU ZAO LA MUHOGO
UTANGULIZI
Muhogo(manica esculentum) ni zao la jamii ya
mizizi kama vile viazi, linalostawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye
mwinuko wa mita 0-1500 toka usawa wa bahari. Zao hili hustawi kwenye maeneo
yanayopata mvua za wastani wa 750mm hadi 1200mm kwa mwaka, hustawi vizuri
kwenye ardhi yenye udongo wa Kichanga usiotuamisha maji.
Mihogo ni
zao muhimu sana kwa Tanzania kutokana na sifa zake za kuvumilia ukame, kustawi
kwenye maeneo yenye rutuba kidogo, hivyo inahitaji gharama ndogo za uzalishaji.
Kwa hali
hiyo zao za Muhogo linaweza kulimwa zaidi na wakulima wadogo wadogo wenye
vipato vidogo huko vijijini.
AINA ZA MIHOGO
Nchini
Tanzania, kuna aina zaidi ya 45 za Mihogo na zaidi ya 80% ya mihogo hii ni ya
asili(Kituo cha utafiti wa mazao ya Kilimo-Naliendele). Hii ina maana kuwa
wakulima wengi wanalima mihogo ya asili.
Mihogo
michungu bado inaendelea kulimwa kwenye jamii zetu kwa sababu haishambuliwi
kirahisi na magonjwa na wadudu, ila pia ni rahisi kuhifadhi baada ya Mavuno.
a.
MIHOGO YA ASILI
Mihogo ya
asili ni ile iliyolimwa miaka mingi iliyopita na kurithiwa vizazi kwa vizazi.
Mihogo hii ina sifa zifuatazo:-
·
Hutoa
mavuno wastani wa Tani 10 hadi 20 kwa hekta.
·
Inaweza
kuhifadhiwa shambani kwa mda mrefu bila kuoza.
·
Huchukua
muda mrefu kukomaa(kufikia hatua ya kuvunwa)
·
Hushambuliwa
kirahisi na magomnjwa kama Michrizi ya
kahawia, batobato na blaiti
·
Hushambuliwa
na wadudu aina ya millibagi
·
Wakulima
wanaijua vizuri , tabia na utunzaji wake.
b.
MIHOGO BORA
Hii ni
mihogo iliyofanyiwa utafiti na wataalamu na kuthibitishwa na Kamati ya Mbegu ya
Taifa kufaa kwa matumizi ya wakulima. Kupitia kituo cha utafiti wa mazo ya
kilimo cha Naliendele, Mtwara mbegu aina ya Naliendele na Kiroba zilifanyiwa
utafiti kukubalika kutumiwa na wakulima wa Mihogo nchini Tanzania.
Sifa za
mbegu hizi ni zifuatazo;-
·
Hutoa
mavuno ya Tani 19-30 kwa hekta.
·
Hustahimili
mashambulizi ya magonjwa kama vile Michirizi
ya Kahawia, Batobato na Blaiti.
·
Hukomaa
kwa kipindi cha Miezi 9 baada ya
kupanda.
MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU KWA ZAO
LA MUHOGO
Zao la
muhogo linashambuliwa na magonjwa makuu mawaili ambayo ni Michrizi ya kahawia/Matekenya na Batobato/ukoma wa majani(cassava mosaic disease), na wadudu
waharibifu kwa zao la Muhogo ni kama wafuatao: Cassava Mealy Bug(CMB), Cassava
Green Mites(CGM), White Scales na Mchwa.
Pia, wanyama
wanaharibu sana mazao ya Mihogo yakiwa shambani, wanyama hawa ni kama vile:
Nguruwe na Panya.
Magonjwa
haya ya zao la mihogo yanasababishwa na virusi(ipomovirus) na kuenezwa kutoka
mmea mmoja na mwinginge kupitia Nzi Mweupe(white
fly) na mdudu aina ya Bemisia afer.
Sehemu za mmea ambazo hushambuliwa na magonjwa haya ni pamoja na Majani, Shina
na Mizizi kulingana na hatua ya ukuaji wa muhogo.
Dalili zake
kulingana na magonjwa niliyoyataja hapo juu ni kama zifuatazo: Rangi ya njano kwenye majani, rangi ya dhambarau/kahawaia kwenye shina,
kufa kwa mizizi ya muhogo, ukuaji
usiolingana wa majani, kujikunja na kupungua umbo kwa majani, kudumaa kwa mmea
na majani machanga kuvimba.
JINSI YA KUZUIA NA KUDHIBITI MAGONJWA
NA WADUDU WAHARIBIFU
·
Kuchagua
mbegu kutoka mmimea isiyo na dalili za ugonjwa.
·
Hakikisha
unapanda mbegu bora za muhogo zinazostahimili uambukizo wa Magonjwa.
·
Kuelewa
dalili za magonjwa kwa ajili ya kuchukua hatua haraka.
·
Kutunza
mbegu bora zinazovumilia magonjwa sana.
·
Kuweka
shamba safi kupunguza visababishi vya magonjwa.
·
Kutumia
dawa za kuulia wadudu waharibifu.
·
Hakikisha
unateketeza mihogo iliyo athirika baada ya mavuno.
UVUNAJI NA USINDIKAJI WA MUHOGO
Mihogo
inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 hadi 12 tangu kupandwa. Inashauriwa
kuvunwa katika kipindi cha Jua kwasababu ukivuna kipindi cha mvua kiwango cha
wanga hupungua.
Usindikaji
bora wa muhogo unafanywa kwa sababu zifuatazo: Kurahisisha/kuharakisha
ukaushaji, Kuondoa sumu(cynanide) iliyoko kwenye baadhi ya aina za mihogo na
Kuongeza thamani(value addition) zao la muhogo kwa kutengeneza unga wa muhogo.
Njia bora za usindikaji wa Muhogo
a.
Kwa kutumia mashine aina ya Grater
Hii hutoa
chembechemebe laini za muhogo amabazoz baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa
kiitwacho “presser” ili kuondoa sumu iliyoko kwenye muhogo. Hii mashine ni
mahususi kwa muhogo mchungu.
b.
Kwa kutumia mashine ya chipper
Mashine hii
hutoa vipande vidogo vidogo(chips) na hutumika hasa kwa ajili ya mihogo
mitamu/baridi.
MATUMIZI YA MUHOGO
·
Muhogo
unaweza kupikwa wenyewe kama chakula au kutengeneza unga
·
Unga
wa muhogo unaweza kutumika kutengeneza vitu vyote vinvyotengenezwa na unga wa
ngano kama vile: Biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.k
·
Pia,
muhogo unaweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa zingine kama vile Wanga.
Imeandaliwa
na Mtaalamu wa Uchumi Kilimo na Biashara
SAMSON
ALFRED SHILA
MTWARA-MANISPAA





0 comments:
Post a Comment