Listening to General Secretary Bankmoon addressing delegates from different countries on the theme of session

Having a lunch with other delegates from different countries day one at UN Geneva-Switzerland(Europe)

The storm ended in 2012. It was the day unspeakable, and the joy unforgettable at Chimwaga Hill Conference: The University of Dodoma-UDOM

With special attention while taking photos at American Embassy in Nairobi Kenya

With the smiling face in Nairobi Kenya at American Embassy :From the left is Dannilo from Mozambique, Anderson from Tanzania, Dr.Katabaro-Tz, and the blogger in the right side Dr.Msoline

Tuesday, 13 December 2016

HII NI YA KWENU WANANDOA

Zifuatazo ni njaa mbili zinazowasumbua wanandoa endapo hawatashibishana.

1. Njaa ya mwanamke ni upendo:

Mwanamke anahitaji upendo kuliko vitu vingine, hata katika vitabu vya dini vinasema; enyi waume, wapendeni wake zenu. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe, mwanaume anatakiwa kujitoa kwelikweli kumpenda mke wake kama tunavyojua upendo ndio falsafa kubwa sana katika maisha ya binadamu, upendo huvumilia, hufadhili, hauhusudu. Hivyo basi njaa ya mwanamke ni kupendwa. Wewe kama mwanaume unatakiwa kumpenda mke wako kwa moyo wako wote bila kujali udhaifu wake. Hii ndio njaa ya wanawake wanahitaji upendo katika maisha ya ndoa.

2. Njaa ya mwanaume ni kuheshimiwa:

Mwanaume njaa yake kubwa ni kuheshimiwa katika maisha ya ndoa. Sasa ikitokea mwanaume anakosa kuheshimiwa na mke wake katika maisha ya ndoa hivyo anakuwa amekosa kushibishwa njaa yake. Na kama akikosa kushiba ndio matatizo huanzia hapo itamlazimu kutafuta kushibishwa njaa yake nje. Hivyo kama wewe ni mwanamke unatakiwa kumshibisha mume wako njaa yake ya kumtii.

Kama wanandoa wanashindwa kushibishana njaa zao, hivyo wanajitengenezea shimo wao wenyewe. Watu wanajisahau sana katika kutimiza majukumu yao katika maisha ya ndoa hatimaye wanaruhusu haki za kibinadamu kuingia maisha ya ndoa, kama wanandoa mkishaingiza haki za kibinadamu katika maisha ya ndoa yaani hamsini kwa hamsini kama wanavyodai lazima mtapoteza mwelekeo tu.

Kwa hiyo kila mtu ana njaa yake kama tulivyoona hapo juu sasa mkishayaingiza mambo haya ya kidunia mtakosa kushibishana njaa zenu.

Mwisho, kila mwanandoa ana wajibu wa kumshibisha mwenza wake, mke akipendwa atashiba njaa yake na mume akiheshimiwa atashiba njaa yake. Kila mtu ana njaa yake hivyo mnatakiwa kushibishana na kupendana katika shida na raha.

0 comments:

Post a Comment