Bwana mmoja aliyepata kuwa tajiri na mwenye mali nyingi. Alikutana na mwanamke, wakapendana sana. Wakaamua kuoana.
Siku ya harusi yao, Bwana yule alimpa mkewe sharti moja. Sharti gumu
sana. Akamwambia: "Ukitaka ndoa yetu idumu, hakikisha uniingilii kwa
jambo lolote nitakalofikiri na kuamua. Ukikiuka sharti hilo, basi
nitakufukuza mara moja nyumbani kwangu. Siku ya kuondoka nitakuruhusu
uchukue kitu kimojs tu ktk mali zote nilizonazo. Ukichague kitu hicho na
uende nacho kwenu".
Ikatokea jioni moja, katikati ya mazungumzo, Bibi yule alitamka: "Hapana sikubaliani na wewe!". Hivyo, alikiuka sharti lile. Bwana yule alikasirika sana. Akatamka kwa hasira:"Unakumbuka sharti langu, ufikili sana kitu kimoja cha kuchagua kilichomo ndani ya nyumba yangu, alfajiri ikifika uanze safari ya kwenda kwa wazazi wako."
Baada ya kuyasema hayo, Bwana yule hakutaka tena kuzungumza na mkewe. Akachukua pombe zake, alianza kunywa, chupa moja baada ya nyingine. Alilewa chakari, alisahau hata kwenda chumbani, akalala kitini.
Mkewe akaomba msaada kwa vijana nyumba ya jirani. Kwa pamoja wakambeba Bwana yule hadi nyumbani kwa wazazi wa mke.
Asubuhi ikafika, Bwana yule alikurupuka usingizini, akajikuta yumo kitandani nyumbani kwa wakwe zake.
Nimefikaje hapa? Aliuliza kwa upole na kwa mshangao. Mkewe akamkumbatia na kumwambia: "Uliniambia siku ya kuondoka nyumbani kwako nichukue kitu kimoja tu, nami nimechukua wewe mpenzi wangu".
Bwana yule alitabasamu na kumpiga busu mkewe. Kisha wakaongozana kurudi nyumbani kwako.

0 comments:
Post a Comment