Listening to General Secretary Bankmoon addressing delegates from different countries on the theme of session

Having a lunch with other delegates from different countries day one at UN Geneva-Switzerland(Europe)

The storm ended in 2012. It was the day unspeakable, and the joy unforgettable at Chimwaga Hill Conference: The University of Dodoma-UDOM

With special attention while taking photos at American Embassy in Nairobi Kenya

With the smiling face in Nairobi Kenya at American Embassy :From the left is Dannilo from Mozambique, Anderson from Tanzania, Dr.Katabaro-Tz, and the blogger in the right side Dr.Msoline

Tuesday, 13 December 2016

WASOMI WA TANZANIA TUNALO LA KUJIFUNZA TOKA WASOMI WA CHINA


Kama kawaida yetu, Team Tibaijuka tunapenda kukujuza juu ya wasomi wa China.
Vijana wengi nchini China wanakataa kwenda kufanya kazi sehemu zilizo nje ya miji. Serikali ya China imejitahidi sana kuboresha maisha ya wafanyakazi wanaopangiwa pembezoni mwa nchi. Serikali inajitahidi kuwapa vivutio zaidi wale wanaokubali kwenda pembezoni mwa nchi. Na pia kuwanyima baadhi ya haki wale wanaogoma kwenda huko vijijini.

Kwa maana nyingine mtu akigoma kwenda huko kijijini, basi maana yake yeye ameamua kuwa MMACHINGA. Kama kuna vitu vinavyoisumbua serikali ya China siyo vyama vya upinzani hata kidogo, bali ni mitandao ya kijamii na wamachinga.

Sehemu kubwa ya WAMACHINGA wa China siyo kama wa kwetu Tanzania. WAMACHINGA wa China ni watu wenye shahada moja na wengine mbili.

Hawa wana umoja mkuvwa sana. Serikali ikitangaza jambo lolote linalowagusa wanakuwa kitu chenye nguvu sana dhidi ya serikali yao.

Busara za viongozi wa China zimewafundisha kwamba, kabla ya kufanya uamuzi wowote mkubwa ni lazima kwanza wafikilie kundi hili, na kujiuliza je uamuzi wa serikali utapokelewaje? Hili ni kundi ambalo kwa kutumia mitandao linaweza kutaarifiana ndani ya robo saa na wote wakagoma kwenda kazini, na hivyo kusimamisha shughuli za uzalishaji kwa siku hiyo.

Lengo langu hapa si kuhamasisha kugoma. Bali kujenga umoja na mtandao wa wasomi ulio imara na kupashana habari mbalimbali za kuinuana kiuchumi.

Kundi la wasomi tena vijana, tuna changamoto nyingi sana. Tusipokuwa wamoja, tusitegemee kumaliza hizi changamoto. Kabla ya kuita mtu asaidie changamoto zetu, basi tuanze sisi wenyewe kwanza.

0 comments:

Post a Comment