Listening to General Secretary Bankmoon addressing delegates from different countries on the theme of session

Having a lunch with other delegates from different countries day one at UN Geneva-Switzerland(Europe)

The storm ended in 2012. It was the day unspeakable, and the joy unforgettable at Chimwaga Hill Conference: The University of Dodoma-UDOM

With special attention while taking photos at American Embassy in Nairobi Kenya

With the smiling face in Nairobi Kenya at American Embassy :From the left is Dannilo from Mozambique, Anderson from Tanzania, Dr.Katabaro-Tz, and the blogger in the right side Dr.Msoline

Wednesday, 1 February 2017

KAINAMLA AUAGA UKAPELA

                               HONGERA SANA KAINAMLA BWENGE

Ilikuwa ni vifijo na nderemo pale Kainamla alipoingia ukumbini kwa miondoko ya aina yake, akiwa na wake Mrs.

                                     Tukimbizane nini salome wangu, hiyo michezo ya jogooo!!
Kainamla akiingia ukumbini kwa mwendo wa kukimbizana, lakini hiyo si michezo ya jogoooo! hataaa, bali waliamua tu.

                                         Kila mtu kwa nafasi yake aliifurahia hii harusi

Kwa kweli tulikula, tukanywa. Ilikuwa ni tumbo lako tu linabeba kiasi gani cha msosi, lakini bado uliruhusiwa kubeba kwuondoka na msosi hadi nyumbani kwako. Nyama, bia, na kila aina ya maanjumati. Kweli, watu walifurahi sana siku hiyo


Mama mzazi akimkaribisha mkamwana. Nyegere waitu, Mabira ndo kwako kwa sasa. Mama katika msisitizo mkubwa

Wapambe nao hawakuwa mbali sana. Walihakikisha tukio linaenda ipasavyo, ndo wakaamua kujiachia kwa pozi dogo tu, lakni lenye ubunifu mkubwa sana.

Mpaka mda huu najiuliza, hizi ni tai au ni nini? Maana muundo huu ndo mara yangu ya kwanza kuuona. Nadhani ni muundo mpya wa tai. Basi muundo umeanza na Kainamla. Kiujumla walipendeza maharusi wetu.
            Shemeji yetu uyooo, kwa tabasamu mwanana! Karibu sana unyamboni. Nyegere mno!
               Maharusi wetu haoo kabla ya harusi wakioneshana upendo na heshima.

Ilikuwa ni harusi kubwa, iliyogharimu kiasi cha shilingi MILIONI 24. Watu walikula, wakanywa. Na watu walitoka kila pembe ya dunia. Ndugu, jamaa, marafiki na wakereketwa walifika kwenye tukio la kaka yangu, rafiki yangu kipenzi Kainamla Bwenge.

Kwa sasa kakaangu ashauaga ukapera. Hongera sana. Na maisha kiujumla kaka anayajua sana. No worries. Kama ni upendo, Kainamla anao upendo mkubwa sana. anajua kuhandle, anajua kupeti peti, anajua kila kitu. Shemjei yangu, hongera kuja kwa Kainamla. Hutojutia maisha yako yote. Umechangua kilicho bora zaidi. Mungu aibariki hii ndoa.

0 comments:

Post a Comment